Sunday, September 22, 2013

ESPERANCE YAMALIZA MAKUNDI KWA USHINDI ASILIMIA MIA MOJA.

KLABU ya Esperance ya Tunisia imefanikiwa kupata ushindi wa ugenini baada ya kuifunga Coton Sport ya Cameroon kwa mabao 2-1 katika mechi za mwisho za makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mabingwa mara mbili wa Afrika wanafukuzia taji lao la tatu la michuano hiyo ikiwa ni miaka miwili pekee imepita toka wanyakuwe taji lingine. Esperace ambao wako katika kundi B tayari walikuwa wameshajihakikishia nafasi ya kusonga mbele kabla ya mchezo huo wakiwa na alama saba zaidi Coton Sport ambao nao pamoja nakipigo hicho lakini walisonga mbele baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi hilo. Coton sasa watakwaana na mshindi wa kundi A ambaye ni Al Ahly katika hatua ya nusu fainali huku Esperance wao wakionyeshana kazi na Orlando Pirates ya Afrika Kusini ambao wameshika nafasi ya pili katika kundi A.

No comments:

Post a Comment