Tuesday, September 3, 2013

BAYERN SI CHOCHOTE BILA RIBERY - BECKENBAUER.

NGULI wa soka nchini Ujerumani, Franz Beckenbauer anaamini kuwa Bayern Munich wasingeshinda mataji masimu uliopita kama asingekuwepo Franck Ribery. Winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Shirikisho la Sola barani Ulaya-UEFA wiki iliyopita kufuatiwa mafanikio aliyopata msimu wa 2012-2013 na Beckenbauer alimpongeza nyota huyo kwa juhudi zake msimu uliopita. Nguli huyo aliuambia mtandao wa FIFA kuwa bila Ribery Bayern wasingeweza kushinda mataji matatu labda wangeweza kushinda moja au mawili. Mzee huyo aliendelea kudai kuwa winga huyo alichangia kwa kiasi kikubwa mafanikio hayo kwasababu ni mmoja ya wachezaji bora kabisa duniani na mwaka huu alikuwa katika kiwango kikubwa.

No comments:

Post a Comment