Tuesday, September 3, 2013

ESSIEN AANZA MAZOEZI KWA MARA YA KWANZA NA GHANA BAADA YA KUPITA MIAKA MIWILI.

KWA mara ya kwanza baada ya kupita miaka miwili, kiungo wa Chelsea Michael Essien amefanya mazoezi na kikosi cha timu ya taifa ya Ghana katika maandalizi ya mechi yao ya Ijumaa ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika jijini Accra. Mara ya mwisho Essien kuitumikia Ghana ilikuwa ni miaka miwili iliyopita kabla ya kustaafu na kuhamishia nguvu zake klabuni baada ya kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yalikuwa yakitishia soka lake. Hata hivyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 alifanya mazoezi ya kukimbia pekee na wenzake na kukaa benchi wakati wachezaji wengine wakicheza na mpira. Wachezaji wengine walioshiriki katika mazoezi hayo ni pamoja na nahodha Asamoah Gyan, Albert Adomah, Rashid Sumaila, Mahatma Otoo, Kwadwo Asamoah, Jonathan Mensah, Razak Braimah, Fatau Dauda, Rabiu Mohammed, Christian Atsu, Mubarak Wakaso and Awal Mohammed. Wachezaji wengine akiwemo Kevin-Prince Boateng wanatarajiwa kuwasili muda wowote ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho ambacho kitahitaji ushindi katika mechi hiyo ili waweze kusonga katika hatua ya mtoano itakayoshirikisha timu 10.


No comments:

Post a Comment