TIMU ya Cape Verde imeendelea kuwashangaza watu baada ya kuiengua Tunisia katika kufuzu michuano ya Kombe la Dunia baada ya kushinda kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa jijini Rades. Katika mchezo huo Tunisia ambao walikuwa nyumbani walikuwa wakihitaji sare ili waweze kuibuka vinara katika kundi lao lakini mabao yaliyofungwa na Platini na Nhuck katika kipindi cha kwanza yalifuta ndoto zao na kupelekea Cape Verde kusonga mbele katika hatua ya mtoano. Kwa upande mwingine Ethiopia nao walifanikiwa kutinga katika hatua ya mtoano baada ya kuifunga Afrika ya Kati kwa mabao 2-1 na kufanikiwa kumaliza wakiwa na alama 13 katika kundi A, alama mbili zaidi ya Afrika Kusini ambao ushindi wao wa mabao 4-1 dhidi ya Botswana haukusaidia. Nchi hizo mbili sasa zitaungana na Algeria, Burkina Faso, Misri, Ghana, Ivory Coast, Nigeria na Senegal katika hatua ya mtoano huku mshindi kati ya Cameroon na Libya na kuungana na nchi hizo ili kutimiza timu 10.
No comments:
Post a Comment