Sunday, September 8, 2013

KESHI AMRUDISHA UBELGIJI SAINTFIET.

KOCHA wa timu ya taifa ya Malawi, Tom Saintfiet amejiuzulu wadhifa wake huo baada ya kikosi chake kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Nigeria katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia uliochezwa jijini Calabar jana. Saintfiet ambaye aliteuliwa Julai 2 mwaka huu na Chama cha Soka cha Malawi-FAM amefafanua kuwa alikuwa na makubaliano na chama hicho mpaka Jumamosi usiku. Kocha huyo raia wa Ubelgiji amedai kuwa lengo lake kubwa akiwa kama kocha wa Malawi ilikuwa ni kuwafunga mabingwa wa Afrika Nigeria huko Calabar kitu ambacho ameshindwa kukitimiza. Akihojiwa mara baada ya mechi hiyo Saintfiet amesema hakuwepo hapo kushinda mechi nyingi bali ni kushinda mechi ya Jumamosi dhidi ya Nigeria hilo ndio lilikuwa lengo lake pekee hivyo kushindwa kwake ni sababu pekee ya kuondoka.

No comments:

Post a Comment