Sunday, September 8, 2013

TOKYO YATEULIWA KUWA MWENYEJI WA OLIMPIKI 2020.

JIJI la Tokyo limechaguliwa kuwa mwenyeji wa michuano ya olimpiki ba paralimpiki 2020 na kuishinda miji ya Istabul, Uturuki na Madrid, Hispania. Mji huo mkuu w Japan ulishinda mzunguko wa mwisho wa kura zilizopigwa na wajumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC katika hafla iliyofanyika jijini Buenos Aires, Argentina. Katika kura hizo Madrid ilienguliwa mapema na kuiacha miji hiyo miwili katika duru la mwisho la kura ambapo Tokyo iliibuka na ushindi kwa kuzoa kura 60 dhidi ya 36 za Istabul. 
Ilikuwa ni sherehe kubwa nchini Japan pamoja na viongozi wa nchi hiyo waliokuwepo kwenye shughuli hiyo wakati rais wa IOC Jacques Rogge ambaye anamaliza muda wake Jumanne ijayo baada ya kuongoza kwa miaka 12, kuitangaza Tokyo kama mwenyeji wa michuano hiyo ya 2020. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Japan kupewa uenyeji wa kuandaa michuano hiyo mikubwa kabisa duniani toka wafanya hivyo mwaka 1964.

No comments:

Post a Comment