Thursday, September 19, 2013

CESAR AVUNJIKA KIDOLE MAZOEZINI.

KLABU ya Queens Park Rangers-QPR imetangaza kuwa golikipa wake Julio Cesar atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane kutokana na majeraha. Cesar alifanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika kidole chake cha mkono wa kushito wakati wa mazoezi Jumanne. Golikipa huyo alitegemewa kuondoka QPR mara baada ya klabu hiyo kushuka daraja masimu uliopita lakini ilishindikana kutokana na kukosa ofa aliyohitaji kutoka timu zingine. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil ndio golikipa chaguo la kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kinanolewa na Luis Felipe Scolari na kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Korea Kusini na Zambia mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment