Thursday, September 19, 2013

WACHEZAJI WAMEKOSA UKOMAVU - MOURINHO.

MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekiri kikosi chake kinakosa ukomavu baada ya kupata kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Basel katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya uliofanyika katika Uwanja wa Stamford Bridge. Katika mchezo huo wenyeji Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Oscar muda mchache kabla ya mapumziko lakini Basel walinikiwa kubadilisha matokeo katika kipindi cha pili kwa mabao yaliyofungwa na Mohamed Salah na Marco Streller. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Mourinho amesema anafikiri kikosi chake kimekosa ukomavu wa kutosha ili kupambana na shinikizo lolote linalotokea katika mechi. Mourinho amesema watakwenda nyumbani wakiwa na huzuni kutokana na kipigo hicho lakini wataamka na kuufanyia kazi udhaifu wao ili kuhakikisha wanafanya vyema katika mechi zao nyingine.

No comments:

Post a Comment