Thursday, September 19, 2013

SUAREZ YUPO FITI - RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema mshambuliaji nyota wa timu hiyo Luis Suarez yuko tayari kurejea katika kikosi cha kwanza baada ya wiki kadhaa za kufanya mazoezi na maandalizi mazuri. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay atamaliza adhabu yake ya kufungiwa mechi 10 kwa kumuuma beki wa Chelsea Branislav Ivanovic April mwaka huu, katika mchezo dhidi ya Southampton Jumamosi. Hiyo itakuwa habari njema kwa Rogders kumtumia nyota huyo katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Manchester United Jumatano ijayo. Lakini meneja huyo alipuuza habari hizo na kudai kuwa hana uhakika kama atamtumia Suarez katika kikosi chake cha kwanza kwenye mchezo huo pamoja na kwamba anajua amefanya mazoezi ya kutosha wakati akiitumikia adhabu yake.

No comments:

Post a Comment