Monday, September 30, 2013

GALATASARAY YAMNYATIA MANCINI.

KLABU ya Galatasaray ya Uturuki imebainisha kuanza mazungumzo ya awali na Roberto Mancini kuhusiana na nafasi ya umeneja iliyopo wazi. Klabu hiyo yenye maskani yake jijini Istanbul ilithibitisha katika ukurasa wake mtandao wa kijamii wa twitter kwamba Mancini alikutana na bodi ya wakurugenzi kwa ajili ya mazungumzo ya kumpa nafasi hiyo. Mancini ambaye ni raia wa Italia atachukua nafasi ya Fatih Terim ambaye alitimuliwa wiki iliyopita baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya. Manchester City walimtimua Mancini Mei mwaka huu ikiwa ni mwaka mmoja toka aiongoze klabu hiyo kushinda taji la kwanza la Ligi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment