Monday, September 30, 2013

WENGER ATOA TAHADHARI DHIDI YA NAPOLI.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amewaonya nyota wa kikosi chake kuwa Napoli sio timu ya kubeza na watakuja kutafuta ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baina ya timu hizo utakaochezwa baadae leo. Arsenal kwasasa wanaongoza Ligi Kuu nchini Uingereza kwa tofauti ya alama mbili baada ya kushinda mechi yao dhidi ya Swansea City Jumamosi iliyopita. Huo unakuwa ushindi wa tano mfululizo kwa Arsenal kati ya mechi sita za ligi walizocheza huku wakipoteza moja dhidi ya Aston Villa. Lakini pamoja na timu yake kuonyesha kiwango kizuri Wenger ameonya kwamba Napoli watakuja kutafuta ushindi na sio matokeo mengine zaidi ya hayo hivyo inabidi wajipange ili kuhakikisha wanakabiliana nao.

No comments:

Post a Comment