Monday, September 30, 2013

REUS AMPA TANO LEWANDOWSKI.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund, Marco Reus amempongeza nyota mwenzake wa timu hiyo Robert Lewandowski kwa kiwango kikubwa ambacho ameonyesha katika siku za karibuni. Lewandowski alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 iliyopata Dortmund dhidi ya Freiburg Jumamosi iliyopita na kufikisha mabao sita katika mechi saba za Bundesliga alizocheza msimu huu. Akihojiwa na mtandao wa klabu hiyo Reus alimsifu nyota huyo ni kudai kwamba ni mmoja kati ya washambuliaji bora kabisa duniani. Reus aliendela kusema kuwa Lewandowski ni aina ya mchezaji ambaye ni vigumu kumkaba wakati ukibakiwa nae peke yake na pia anajua kujiweka katika nafasi nzuri za kufunga.

No comments:

Post a Comment