Tuesday, September 24, 2013

ISTANBUL YAITISHIA WEMBLEY KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KUANDAA MICHUANO YA EURO 2020.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kinaamini kuwa jiji la Istanbul liko mstari wa mbele katika mbio za kuwania nafasi ya kuandaa mechi za nusu fainali na fainali ya michuano ya Ulaya 2020. Katibu mkuu wa FA, Alex Horne amesema jijini hilo ndio watakuwa wapinzani wakubwa wa Wembley katika kuandaa mechi hizo baada ya Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kutangaza nchi 32 ambazo zimeonyesha nia ya kuandaa mechi hizo. Horne amesema baada ya Istanbul kupoteza nafasi ya kuandaa michuano ya olimpiki 2020 kwa Tokyo anadhani watapewa kipaumbele katika michuano ya hiyo. Mapema mwaka huu UEFA ilifikia maamuzi ya kuandaa michhuano hiyo katika miji 13 tofauti barani Ulaya badala ya nchi moja kama ilivyozoeleka hapo awali.

No comments:

Post a Comment