MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Miroslav Klose amefanikiwa kufikia rekodi ya mabao 68 iliyowekwa na Gerd Muller baada ya kushinda bao katika dakika ya 34 kwenye mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ya kundi C dhidi ya Austria jana. Klose ambaye anasifika kama mshambuliaji anayejua kujipanga vizuri wakati timu yake ikishambulia, allifunga bao hilo maridadi baada ya kupokea pasi kutoka upande wa kulia iliyopigwa na Thomas Mueller. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 hiyo inakuwa mechi yake ya 129 toka aitwe kwa mara ya kwanza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani miaka 12 iliyopita. Mueller mwenye aliiweka rekodi hiyo ya kufunga mabao hayo kwa Ujerumani mwaka 1974.
No comments:
Post a Comment