DEREVA nyota wa timu ya Red Bull, Sebastian Vettel amefanikiwa kumpita Fernando Alonso wa Ferrari na kuongoza majaribio ya mwisho ya michuano ya langalanga ya Grand Prix ya Italia. Vettel alimpita Alonso ambaye ni hasimu wake katika kugombea taji la dunia kwa sekunde 0.283 huku dereva mwenzake wa timu hiyo Mark Webber akishika nafasi ya tatu. Mwingereza Lewis Hamilton wa timu ya Marcedes alikamata nafasi ya nne mbele ya Sergio Perez wa McLaren aliyeshika nafasi ya tano akifuatiwa na dereva wa Rosso, Danile Ricciardo ambaye mwaka ujao atakuwa timu moja na Vettel. Mpaka sasa msimamo wa madereva hao katika kuwania taji la dunia Vettel bado anaongoza akifuatiwa na Alonso huku Hamilton na Kimi Raikkonen wa Lotus wakifuatia kwa karibu katika nafasi ya tatu na nne.
No comments:
Post a Comment