Sunday, September 22, 2013

NILIOGOPA KWENDA KUKAA BENCHI CITY - ERIKSEN.

NYOTA mpya wa klabu ya Tottenham Hotspurs, Christian Eriksen amekiri kuwa aliitosa klabu ya Manchester City kwasababu alikuwa anataka kuepuka kukaa benchi. Eriksen ameanza vyema maisha mapya White Hart Lane na kuwashangaza mashabiki katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Norwich na kufunga bao lake la kwanza akiwa na klabu hiyo katika mchezo wa Europa League dhidi ya Tromso. Nyota huyo amekiri kuwa vilabu vingi vikubwa vya Ligi Kuu nchini Uingereza vilikuwa vikimmendea kabla ya kwenda Spurs na kubainisha kuwa City ndio klabu iliyokaribia kumsajili. Eriksen aliendelea kudai kuwa ilimchukua muda kwenda Uingereza kwasababu alikataa mara kadhaa na mwaka jana City walitaka kumsajili lakini alisita kwasababu hakuwa na uhakika wa kucheza akienda huko.

No comments:

Post a Comment