Friday, September 27, 2013

SERENA WILLIAMS KUMALIZA MWAKA AKIWA KINARA.

MWANADADA nyota katika tenisi, Serena Williams wa Marekani anatarajiwa kumaliza mwaka akiwa kinara katika orodha za ubora wa mchezo huo kwa upande wa wanawake baada ya kufanikiwa kushinda mataji mawili ya Grand Slam mwaka huu. Williams mwenye umri wa miaka 32 alipoteza mechi nne pekee kwa mwaka huu na kushinda mataji tisa ikiwemo michuano ya wazi ya Ufaransa na Marekani. Hii ni mara ya tatu kwa mwanadada huyo kukaa kileleni kwenye orodha hiyo kwenye kalenda ya mwaka. Williams amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kushikilia nafasi hiyo wakati alipomng’oa Victoria Azarenka wa Belarus Februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment