Friday, September 27, 2013

WENGER KUENDELEA KUINOA ARSENAL.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa atakuwa tayari kusaini mkataba mpya na timu hiyo baada ya mmiliki wake Stan Kroenke kuonyesha nia ya kuendelea kumhitaji mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 63. Mkataba wa sasa wa Wenger unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini mwenyewe amesema hana haraka ya kuanza mazunguzo ya mkataba mpya. Lakini Wenger akihojiwa mara baada ya Kroenke kuzungumza nia ya klabu kumuongeza mkataba alidai anaipenda klabu hiyo na kutania kwamba atafurahi kama atakaa hapo milele. Wenger pia alimshukuru bosi wake huyo kwa kumpa heshima hiyo na kuonyesha kumuamini lakini akarudia kauli yake kwamba angependa kufanya kuisadia klabu hiyo kufanya vizuri msimu huu na hayo mengine yatafuata baadae. Arsenal inatarajia kusafiri kwenda Wales mwishoni mwa wiki hii kwenda kukwaana na Swansea City katika mechi ya Ligi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment