Sunday, October 27, 2013

ANCELOTTI AMKINGIA KIFUA BALE.



MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amemkingia kifua Gareth Bale pamoja na kiwango cha chini alichoonyesha katika mchezo dhidi ya Barcelona ambao walipoteza kwa mabao 2-1. Nyota huyo mwenye miaka 24 alipangwa katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo ikiwa ni mara ya pili msimu huu. 
Ancelotti amesema Bale alicheza vyema katika muda wote katika mchezo huo pamoja na kwamba walipoteza. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mashabiki wa Madrid wanapaswa kumpa muda zaidi nyota huyo azoee kuliko kuanza kumkatisha tamaa kwa kumponda hivi sasa.

No comments:

Post a Comment