Monday, October 28, 2013

TOURE AKUTANA NA WEBB.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amekutana na maofisa wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kujadili tuhuma kuwa alifanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliofanyika nchini Urusi wiki iliyopita. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikutana na makamu wa rais wa FIFA, Jeffrey Webb katika Uwanja wa Stamford Bridge siku ambayo City walifungwa na Chelsea kwa mabao 2-1. Msemaji wa City alithibitisha wawili hao kukutana lakini alikataa kuzungumzia masuala ambayo walijadili katika kikao chao. Webb pia ni rais wa CONCACAF na kiongozi wa kikosi kazi cha FIFA kinachopambana na masuala ya ubaguzi katika soka.

No comments:

Post a Comment