RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter anataka adhabu kali zaidi ili kupambana na ubaguzi katika soka ikiwemo adhabu ya kuondoa timu mashindanoni au kuwakata alama. Kauli ya Blatter imekuja kufuatia Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuanza uchunguzi dhidi ya klabu ya CSKA Moscow baada kiungo wa Manchester City Yaya Toure kulalamika kufanyiwa vitendo vya kibaguzi na mashabiki. Blatter amedai faini inayotozwa na timu kucheza bila mashabiki inaonekana ni adhabu isiyotosheleza kwasasa. Rais huyo aliendelea kudai kuwa kama kweli wanataka kutokomeza suala hilo michezoni basi inapaswa adhabu kama kuondoa timu katika mashindano husika au kuzikata alama ziongezwe ili kudhibiti mashabiki wasio na adabu.
No comments:
Post a Comment