Sunday, October 27, 2013

INIESTA KUONGEZA MKATABA BARCELONA.

KIUNGO mahiri wa klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amebainisha kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo katika siku za karibuni baada ya kuisaidia timu hiyo kuwafunga mahasimu wao Real Madrid kwa mabao 2-1 jana. Iniesta ndiye alikuwa nyota katika mchezo huo baada ya kusaidia mabao hayo yaliyofungwa kwa umaridadi na Neymar katika kipimndi cha kwanza na lingine la Alex Sanchez. Kulikuwa na tetesi kuwa Iniesta anaweza kumfuata golikipa wa timu hiyo Victor Valdes ambaye alidai kuwa hawezi kuongeza mkataba wa kuinoa klabu hiyo. Akizungumza baada ya mchezo huo Iniesta amesema anafuraha kuwepo hapo na anataka kubakia ndio maana ameamua kuongeza mkataba wake mapema iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment