Sunday, October 27, 2013

VILABU UFARANSA KUFANYA MGOMO MWEZI UJAO.

VILABU vya soka nchini Ufaransa vitafanya mgomo mwezi ujao kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kulalamikia mipango ya serikali kuwatoza kodi ya asilimia 75 wanaopata mapato makubwa. Mgomo huo wa kwanza katika soka la Ufaransa tangu mwaka wa 1972 unatarajiwa kuandaliwa katika wikiendi ya mwisho ya Novemba baada ya vilabu hivyo kupiga kura kwa kauli moja dhidi ya mpango huo wenye utata wa Rais wa Ufaransa Francois Hollande wa kutoza kiwango kikubwa cha kodi. Rais wa chama cha vilabu vya soka vya Ufaransa – UCPF Jean-Pierre Louvel amesema hakutakuwa na mechi yoyote ya ligi Novemba 29 na Desemba 2. Chini ya mapendekezo hayo, makampuni badala ya wachezaji yatahitajika kulipa kiwango cha juu cha kodi kwa niaba ya wafanyakazi wao ambao ni wachezaji ambacho kinazidi euro milioni moja.


No comments:

Post a Comment