Sunday, October 27, 2013

EL SHAARAWY ATAKA KUMKIMBIA BALOTELLI MILAN.


MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya AC Milan, Stephen El Shaarawy amedai kutaka kuondoka katika klabu hiyo kwenda kusaka maisha mapya katika timu nyingine ili aweze kupata nafasi ya kucheza. Uamuzi wa kinda huyo mwenye miaka 20 unazifanya klabu za Chelsea, Tottenham Hotspurs na Arsenal kuingia vitani lakini Liverpool inaelezwa ndio wana nafasi kubwa zaidi ya kumnyakuwa nyota huyo.  El Shaarawy ambaye alifunga mabao 16 msimu uliopita amekuwa akipata wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza toka Mario Balotelli atue San Siro. Wamiliki wa Liverpool wanapanga mipango ya kununua wachezaji wadogo na El Shaarawy anaonekana kuwemo kwenye mipango hiyo.

No comments:

Post a Comment