BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, William Gallas amekubali mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na klabu ya Perth Glory na kuongeza idadi ya wachezaji nyota waliojiunga na Ligi Kuu nchini Australia maarufu kama A-League katika siku za karibuni. Gallas mwenye umri wa miaka 36 ambaye ameichezea Ufaransa mechi 84 na pia kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 na 2010, amekuwa bila timu toka amalize mkataba wake wa miaka mitatu na klabu ya Tottenham Hotspurs Julai mwaka huu.
Ofisa Mkuu wa Perth, Jason Brewer amesema ni faraja kwa klabu hiyo kuweza kumvutia mchezaji kama Gallas na ni mategemeo yao ligi yao inaweza kukua zaidi na kuwavutia wachezaji nyota wengi zaidi duniani. Mbali na Gallas nyota wengine wanaokipiga A-League ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Italia Alessandro Del Piero, Shinji Ono wa Japan na mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Emile Heskey.
No comments:
Post a Comment