MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba alifunga bao bao katika ushindi wa mabao 3-1 iliyopata nchi yake dhidi ya Senegal katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia hatua ya mtoano mkondo wa kwanza. Katika mchezo huo uliopigwa jijini Abidjan, wenyeji Ivory Coast ambao waliita nyota wao wote wanaocheza Ulaya walionekana kumiliki vyema mchezo huo toka kipindi cha kwanza hivyo kuwanyima nafasi wapinzani wao kufurukuta pamoja na wao pia kusheheni nyota wanaocheza katika vilabu mbalimbali barani Ulaya. Drogba alifunga bao hilo kwa penati katika ya tano ya mchezo huo huku bao la pili likiwa la kujifunga wenyewe na Solomon Kalou alikamilisha karamu hiyo kwa kufunga bao la tatu mapema wakati wa kipindi cha pili. Vurugu katika mchezo ambao Senegal waliwakaribisha Ivory Coast katika mchezo wa kufuzu wa michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka jana umepelekea nchi hiyo kufungiwa mwaka mmoja hivyo itacheza na Ivory Coast katika mechi ya mkondo wa pili jijini Casablanca, Morocco Novemba 16 mwaka huu. Katika mchezo mwingine Burkina Faso nao walifanikiwa kupiga hatua moja kuelekea katika michuano hiyo baada ya kuigaragaza Algeria kwa mabao 3-2.
No comments:
Post a Comment