Monday, October 14, 2013

LEWANDOWSKI AITAMANI LIGI KUU UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Robery Lewandowski ameweka wazi nia yake ya siku moja kucheza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye mkataba wake na Dortmund unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alidai Septemba mwaka huu kwamba atasaini mkataba Bayern Munich Januari mwakani kabla ya kukanusha taarifa hizo baadae. Meneja wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alikuwa akimwinda nyota huyo katika kipindi cha majira ya kiangazi lakini ilishindakana baada ya Leandowski kuonyesha nia ya kwenda Bayern. Akihojiwa Lewandowski amesema anaweza kusaini mkataba na klabu yoyote ifikapo Januari lakini akakanusha kuwa hakuwahi kusema kwamba atasaini na Bayern. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kimetokea suala la kutoelewana na kukiri kuwa ni kweli alifanya mazungumzo na Ferguson mwaka jana lakini hawakuzungumzia masuala ya uhamisho.

No comments:

Post a Comment