Monday, October 14, 2013

MARADONA AENDELEZA BIFU NA NCHI YAKE.

NGULI wa zamani wa Soka wa Argentina, Diego Maradona ameendelea na ugomvi wake wa kipindi kirefu na nchi hiyo baada ya kutangaza kuwa hataiunga mkono timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Argentina ambayo itashiriki michuano ya Kombe la Dunia huko Falme za Kiarabu-UAE. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Napoli ya Italia, bado hajamaliza tofauti zake na Chama cha Soka cha Argentina-AFA toka alipotimuliwa nafasi ya ukocha katika timu ya wakubwa ya nchi hiyo baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2010. Maradona kwasasa ni mshauri wa klabu ya Deportivo Riestra ya nchini kwake na pia ni balozi wa michezo wa Dubai baada ya kuacha kuifundisha klabu ya Al Wasl mwaka jana. Akizungumza na waandishi wa habari, Maradona amesema ataiunga mkono timu ya taifa ya UAE katika michuano hiyo na sio Argentina kwasababu ya matatizo yake na AFA.

No comments:

Post a Comment