Sunday, October 13, 2013

MISRI YAIHAKIKISHIA FIFA USALAMA WA KUTOSHA.

CHAMA cha soka cha Misri-EFA kimelihakikishia Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kuwa wameweka ulinzi wa uhakika katika mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia hatua ya mtoano dhidi ya Ghana. Ghana iliandika barua FIFA kuomba mchezo wao huo kuhamishwa na kuchezwa nje ya Misri kutokana na matatizo ya kiusalama hivyo kuwafanya EFA kutoa uhakika wa usalama katika mechi hiyo. Msemaji wa EFA Azmy Megahed amesema tayari wamehakikishiwa usalama kutoka wizara ya mambo ya ndani na jeshi la Misri hivyo hakuna kitu cha kuhofia katika mchezop huo. Megahed amesema mbali na kuhakikishiwa usalama lakini pia mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa El Defea El Gawe ambao unamilikiwa na jeshi la nchi hiyo. Misri itakwaana na Ghana Novemba 19 jijini Cairo katika mchezo wa mkondo wa pili ya kufuzu michuano ya Kombe ya Kombe la Dunia huku mchezao wa mkondo wa kwanza ukitarajiwa kuchezwa Jumanne katika Uwanja wa Baba Yara jijini Kumasi.

No comments:

Post a Comment