Thursday, October 10, 2013

MASHABIKI WANAUME WAFUNGIWA MECHI ZA BESIKTAS.

KLABU ya Besiktas ya Uturuki italazimika kucheza mechi nne za nyumbani bila ya mashabiki wanaume baada ya rufani yao kutupiliwa mbali na Kamati ya Usuluhishi nchini humo. Mechi kati ya Besiktas na timu za Rizespor, Kardermir Karabukspor, Torku Konyaspor na Sivasspor zitahudhuriwa na mashabiki wanawake na watoto pekee kufuatiwa wanaume kuzuiwa kutokana na vurugu mwishoni mwa mechi dhidi ya Galatasaray mwezi uliopita. Mechi baina ya timu hizo ilivunja rekodi ya mahudhurio na kufikia 76,712 lakini iliingia dosari kwa wachezaji kukimbia katika vyumba vyao vya kubadilishia nguo kujificha baada ya mamia ya mashabiki kuvamia uwanja mwishoni mwa mchezo. Kocha wa Besiktas alipewa adhabu ya kufungiwa mechi tatu na Shitikisho la Soka la nchi hiyo kufuatia kumshambulia mwamuzi wakati klabu hiyo ilitozwa faini ya euro 21,000 kwa kushindwa kuwadhibiti mashabiki wao.

No comments:

Post a Comment