Thursday, October 10, 2013

WENGER AUNGA MKONO KAULI YA WILSHERE.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameunga mkono madai ya kiungo Jack Wilshere kuwa Waingereza pekee ndio wanapaswa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo. Mshambuliaji wa Manchester United mzaliwa wa Ubelgiji Adnan Januzaj anaweza kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo kama akichukua uraia. Akiulizwa kuhusiana na suala hilo Wilshere mwenye umri wa miaka 21 amesema kama mtu ameishi Uingereza kwa miaka mitano haimfanyi kuwa mwingereza. Kauli ya nyota huyo ilizua mjadala mkubwa lakini Wenger ameonyesha kukubaliana na maneno ya kiungo wake huyo. Hata hivyo Wilshere ambaye amecheza mechi 10 katika timu ya taifa ya Uingereza amesema kauli yake haijamlenga Januzaj ambaye meneja wa Uingereza Roy Hodgson alithibitisha kufuatilia nyendo zake.

No comments:

Post a Comment