Wednesday, October 9, 2013

NANI KUTANGULIA BRAZIL WIKIENDI HII?

WAKATI kampeni za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 zikifikia hatua ya mwisho baadhi ya timu mwishoni mwa wiki hii zinaweza kujihakikishia nafasi kushiriki michuano hiyo mwakani. Wenyeji Brazil tayari wameungana na wawakilishi kutoka bara la Asia ambao ni Japan, Australia, Iran na Korea Kusini huku Ulaya tayari kukiwa na vigogo Uholanzi na Italia pamoja na Marekani, Costa Rica na Argetina. Katika siku chache zijazo timu zingine kutoka mataifa ya Afrika, Ulaya, Amerika Kaskazini na Amerika Kusini nazo pia zinaweza kujihakikishia nafasi katika michuano hiyo. Kwa upande wa Ulaya nchi za Ubelgiji, Ujerumani, Switzerland, Urusi, Bosnia-Herzegovina na Hispania zinaweza kujihakikishia nafasi ya kwenda Brazil kama zikishinda michezo yao ya Ijumaa. Wakati Upande wa Amerika Kusini nchi za Colombia, Chile, Uruguay na Ecuador zote zinaweza kufuzu michuano hiyo kama wakishinda mechi zao, huku Honduras nao wakiwa na uwezo wa kuwa nchi ya tatu kwa upande wa Concacaf kufuzu michuano hiyo kama wakiifunga Costa Rica Ijumaa hii. Wikiendi pia kutakuwa na mechi za mkondo wa kwanza za mtoano kwa uapnde wa Afrika ambapo Burkina Faso wataonyeshana kazi na Algeria, Ivory Coast na Senegal, Ethiopia na Nigeria, Tunisia dhidi ya Cameroon na Ghana wataikaribisha Misri.

No comments:

Post a Comment