MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Barceona, Neymar amekanusha mapendekezo kuwa amelazimika kubadili aina ya uchezaji wake ili aweze kuendana na aina ya uchezaji wa timu yake hiyo mpya. Neymar mwenye umri wa miaka 21 amekuwa chini ya uangalizi wa karibu toka atue Camp Nou akitokea klabu ya Santos ya Brazil huku nguli wa soka Johan Cruyff akidai kuwa nyota huyo hawezi kucheza pamoja na Lionel Messi. Neymar amekuwa katika kiwango kizuri wakati ambapo Messi hayupo kikosini na kutoa mchango mkubwa katika mechi za wiki iliyopita dhidi ya Celtic na Valladolid. Akihojiwa Neymar alikanusha kubadili aina uchezaji na kudai kuwa bado ni mchezaji yuleyule anayecheza kama alivyozoea lakini kwasasa mambo yanamuendea vyema. Nyota huyo amesema haijalishi anacheza Hispania au Brazil jambo la muhimu kwake ni kuongeza kiwango chake kama mchezaji. Kwasasa nyota huyo yuko katika majukumu ya kimataifa ambapo Brazil inatarajia kukwaana na Korea Kusini jijini Seoul Jumamosi.
No comments:
Post a Comment