RAIS wa Shirikisho la Soka baani Ulaya-UEFA Michel Platini amesema katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa soka lazima liongoze harakati za kupinga uabaguzi wa rangi ndani na nje ya uwanja. Kutoka na mchezo wa soka kupendwa na mashabiki wengi zaidi dunia, Platini anadhani mchezo huo utakuwa na nafasi kubwa ya kutokomeza ubaguzi. Platini amesema kutokana na umaarufu mkubwa uliopo katika soka ndio kuna wajibu wa kuongoza kampeni hizo. Katika miaka ya karibuni, UEFA pamoja na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limeongeza juhudi za kupambana na ubaguzi wa rangi michezoni na mojawapo ya adhabu zilizoongezwa ni pamoja na faini ya kiasi kikubwa cha fedha na kucheza katika viwanja vitupu kwa ajili ya vilabu na timu za taifa ambazo amashabiki wake watakutwa na hatia ya vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment