MENEJA wa klabu ya Queens Park Rangers-QPR, Harry Redknapp amesema maofisa wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA hawana uelewa wa kutosha unaowawezesha kuchagua kocha bora kwa ajili ya timu ya taifa ya nchi hiyo. Redknapp alitoa mawazo yake wakati Roy Hodgson alipochaguliwa kuchukua nafasi ya Fabio Capello aliyejiuzulu Mei mwaka jana. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 alikaririwa na gazeti Daily Mail akidai kuwa haamini kama FA wanaweza kuteua meneja mzuri kwa ajili ya kuliongoza taifa hilo kwenye mashindano makubwa. Redknapp aliendelea kudai kuwa hana tatizo lolote na Hodgson baada ya uteuzi wake lakini amesisitiza kuwa yeye ndio alikuwa chaguo la mashabiki na wachezaji kwenye kinyang’anyiro hicho.
No comments:
Post a Comment