KAMATI ya maandalizi ya michuano ya Kombe Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022, imedai kufanya mazungumzo na shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International. Hatua hiyo imekuja kufuatia shirika hilo kudai kuwa kampuni za ujenzi za nchi hiyo zinawanyanyasa wafanyakazi wa kigeni. Kamati hiyo imedai kuwa itashughulikia suala hilo ili kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata haki yao bila ya kunyanyaswa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Kamati iliendelea kudai kuwa kampuni za ujenzi itabidi kukubaliana na sheria mpya za ustawi wa wafanyakazi watakazoweka kwasababu wanatambua mchango wa Amnesty.
No comments:
Post a Comment