MMILIKI wa klabu ya Liverpool John W Henry ametoa ndege yake binafsi kwa ajili ya kuharakisha ujio Luis Suarez kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wao Everton Jumamosi. Kwasasa Suarez yuko nchini Uruguay katika akiitumikia timu yake ya taifa katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya mtoano kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani dhidi ya Jordan unaotarajiwa kuchezwa kesho.
Kwa upande mwingine unaweza sema Uruguay wameshafuzu michuano hiyo kwani katika mechi ya mkondo wa kwanza waliibugiza Jordan kwa maba 5-0. Liverpool inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Everton Jumamosi mchana katika Uwanja wa Goodison Park na ili kuhakikisha mshambuliaji anapata muda wa kupumzika wa kutosha, Henry ameamua kumtumia usafiri huo binafsi ili kumuwahisha.
No comments:
Post a Comment