TIMU ya taifa ya Uholanzi imefanikiwa kumaliza mwaka bila kufungwa mechi hata moja baada ya kutoka sare ya bila ya kufungana na Colombia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Amsterdam. Uholanzi ilifanikiwa kucheza pungufu na wachezaji 10 pekee kwa karibu saa moja baada ya Jeremain Lens kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 35 huku pia wakiwakosa Sien de Jong na Rafael van der Vaart walioumia kabla ya mapumziko. Kukosekana kwa wachezaji hao huku mmoja akitolewa nje moja kwa moja kuliwapunguza makali Uholanzi ambao walikuwa wakicheza nyumbani na kuwafanya kutumia muda mwingi wa mchezo kujilinda. Uholanzi ambayo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Japan Jumamosi iliyopita, imeshinda mechi saba na kutoa sare tano katika mechi 12 walizocheza mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment