BILIONEA wa Uingereza ambaye anamiliki hisa katika klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov ametetea wageni wanaomiliki klabu za Ligi Kuu akidai kuwa ni jambo zuri kwa soka la nchi hiyo. Bilionea huyo amesema kuongeza kwa wamiliki kutoka nje ya nchi hiyo hakuna maana kuwa kutabadili muonekano wa soka la nchi hiyo. Na wakati akiisifia Arsenal kwa kuanza msimu vyema bilionea huyo amedai kuwa pia ana haki ya kukosoa bodi ya klabu hiyo kama ataona hawafanyi mambo kwa ufasaha. Bilionea huyo raia wa Urusi ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri unafikia paundi bilioni 13, ametumia zaidi ya paundi milioni 200 kwa zaidi ya miezi ili kununua asilimia 30 ya hisa za klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment