NYOTA wa mpira wa kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili utakaomfanya kuweka rekodi ya kuichezea Los Angeles Lakers kwa misimu 20. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35 anakuwa mchezaji wa kikapu aliyecheza timu moja katika Ligi Kuu ya Kikapu nchini humo-NBA kama akisaini mkataba huo mpya. Kuna taarifa kuwa Bryant atakatwa kiasi cha paundi milioni 3.71 lakini ataendelea kubakia kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika ligi hiyo akiwa anakunja kitita cha paundi milioni 15 kwa mwaka. Mtendaji Mkuu wa Lakers, Mitch Kupchak amesema nia na madhumuni ya kumuongeza mkatba nyota huyo ni kuhakikisha anastaafu akiwa hapo. Bryant ambaye ameshinda taji la NBA maera tano akiwa na Lakers, hajacheza meci yoyote toka msimu huu uanze kutokana na majeruhi lakini tayari ameanza mazoezi.
No comments:
Post a Comment