VIONGOZI wa klabu ya Schalke ya Ujerumani wameilaumu Ghana baada ya kiungo wao mahiri Kevin-Prince Boateng kushindwa kuitumikia timu hiyo katika mchezo wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Akiwa anaiwakilisha nchi yake kwa mara ya kwanza toka atangaze kustaafu soka la kimataifa Boateng aliifungia Ghana bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Misri ambao uliwawezesha kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Pamoja na hayo kocha wa Schalke Jens Keller amesema toka mchezaji huyo aende Ghana wiki mbili zilizopita hawajaridhishwa na kiwango chake na hawajua ni kitu gani kimemsibu huko. Mbali na Keller kulalamikia hilo pia mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Horst Heldt alidai kuwa safari ya mchezo huyo kwenda Ghana imemharibia badala ya kumjenga na andependa kama angeahirisha safari hiyo.
No comments:
Post a Comment