VINARA wa Ligi Kuu nchini Uingereza, klabu ya Arsenal imepata ahueni baada ya winga wao mahiri Theo Walcott kurejea tena katika kikosi cha timu hiyo katika mchezo dhidi ya Southampton utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Emirates. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amepongeza uwepo wa nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza aliyejiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 16 mwaka 2006 baada ya kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara msimu huu. Wenger amesema anapomkosa mchezaji kama Walcott huwa inakuwa tatizo katika kikosi chake kutokana na umahiri na umakini wake anakuwa karibu na lango la adui. Hata hivyo Wenger aliendelea kudai kuwa hawezi kumtumia nyota huyo moja kwa moja kwasababu ndio kwanza ametoka kwenye majeruhi hivyo ataangalia wakati unafaa kumtumia kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi.
No comments:
Post a Comment