Wednesday, December 18, 2013

AGUERO HATARINI KUIKOSA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero kuna uwezekano wa kukosa mchezo Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona baada ya kuumia msuli wa kigimbi. Meneja wa City Manuel Pellegrini alithibitisha kuumia kwa nyota huyo katika mchezo ambao timu yake ilishinda kwa mabao 6-3 dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita ambapo alidai kuwa naweza kukosekana uwanjani kwa kipindi cha miezi nane. Pellegrini amesema kwa mujibu wa madaktari Aguero anaweza kukaa nje kwa muda wa mwezi mmoja au inaweza kuwa wiki nane. Kama nyota huyo akikaa nje kwa wiki nane anatkosa mechi 12 ikiwemo na mchezo dhidi ya Barcelona utakaochezwa Februari 18 mwakani.

No comments:

Post a Comment