KLABU ya Liverpool imeanza hatua ya kwanza ya mazungumzo katika kuhakikisha inambakisha Luis Suarez kwa mkataba unaoweza kuvunja rekodi ya klabu hiyo. Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo, Ian Ayre alisafiri kwenda Barcelona kufanya mazungumzo na wakala wa Suarez, Pere Guardiola jana ingawa bado hawajampa ofa ya mkataba mpya lakini mazungumzo hayo yameonyesha nia ya Liverpool kuhitaji huduma ya nyota huyo. Inaonekana Liverpool wako tayari kumlipa nyota huyo kitita zaidi ya paundi milioni 130,000 kwa wiki ili kubakisha Anfield kwa mkataba wa muda mrefu. Suarez mwenye umri wa miaka 26 amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu toka amalize adhabu yake ya kumng’ata beki beki wa Chelsea Branislav Ivanoic ambapo amefunga mabao 17 katika mechi 11 alizocheza na kuifanya Liverpool kushika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment