Wednesday, December 18, 2013

MARTINO AMPA NEYMAR SIKU 10 ZA KULA BATA KWAO.

MENEJA wa klabu ya Barcelona, Gerardo Martino amebainisha kumpa likizo Neymar ya kwenda kwao Brazil kwa madhumuni ya kumpa mapumziko zaidi. Nyota huyo alifurahia mapumziko aliyopata baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Martino anaamini Neymar anahitaji mapumziko zaidi baada ya kucheza mechi 23 toka atue barani Ulaya msimu huu. Neymar hatakuwemo katika kikosi cha Barcelona kitakachopambana na Getafe mwishoni mwa wiki akitumikia adhabu hivyo Martino ameona ni vyema akampa nyota huyo mapumziko ya mapema. Nyota huyo mwenye miaka 21 amefunga mabao 11 na kutoa pasi za mabao 10 katika mashindano yote msimu huu.

No comments:

Post a Comment