GOLIKIPA wa kimataifa wa Nigeria, Vincent Enyeama ameeleza nia yake kuataka kubakia kwa kipindi kirefu kwenye klabu ya Lille ya Ufaransa. Enyeama alipewa mkataba wa miaka miwili wa nyongeza na klabu hiyo Jumatatu baada ya kucheza mechi 11 bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa katika Ligi Kuu nchini humo maarufu kama Ligue 1. Wakiogopa tahadhari ya vilabu vingine vilivyokuwa vikimmendea kipa huyo, Lille mara moja walimsainisha mkataba mwingine ambao utamuweka hapo mpaka 2017. Enyeama ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha Nigeria kilichonyakuwa kombe la Mataifa ya AFrika mwaka 2012 amesema anafurahishwa kuwepo klabuni hapo ndio maana amekubali kusaini mkataba mwingine.
No comments:
Post a Comment