WENYEJI wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, klabu ya Raja Casablanca ya Morocco wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuichabanga Auckland City ya New Zealand ambao ni mabingwa wa Oceania. Walikuwa ni wenyeji ndio waliotangulia kupata bao dakika moja kabla ya mapumziko nao ambalo lilifungwa na Mouhssine Iajour kabla ya Fijian Roy Krishna kuisawazishia bao Auckland mapema kipindi cha pili. Bao la ushindi la Casablanca katika mchezo huo lilifungwa dakika za majeruhi na Abdelilah Hafidi hivyo kuwapeleka wenyeji moja kwa moja katika robo fainali ambapo watakwaana na Monterrey ya Mexico ambao ni mabingwa wa CONCACAF. Raja Casablanca ambao walimfukuza kocha wao Mohamed Fakhir na nafasi yake kuchukuliwa na Faouzi Benzarti wa Tunisia wiki iliyopita wamefuzu kucheza michuno hiyo wakiwa kama wenyeji.
No comments:
Post a Comment