MCHEZAJI nyota wa klabu ya Bayern Munich, Thomas Muller anadhani kipigo cha mabao 3-2 walichopata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya dhidi ya Manchester City kimeonyesha kuwa wachezaji wa timu hiyo sio mashine. Bayern walionekana kumudu mchezo huo kwa kupata mabao mawili ya mapema yaliyofungwa na Muller na Mario Gotze lakini City walibadilika na kurejesha mabao yote ambayo yalifungwa na David Silva, Aleksandr Kolarov na la ushindi lililofungwa na James Milner. Muller amesema kipigo hicho kimeonyesha kuwa na wao ni binadamu hivyo kuna muda wanafanya makosa kama waliyoyafanya na kupekea kufungwa katika mchezo ambao tayari walikuwa wakiongoza. Pamoja na kipigo hicho, Bayern bado wameendelea kushikilia usukani wa kundi D na City wako katika nafasi ya pili.
No comments:
Post a Comment