Wednesday, December 11, 2013

ROONEY ACHOMOA TENA MAZUNGUMZO YA MKATABA MPYA UNITED.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amekataa tena kuanza mazungumzo na klabu hiyo juu ya mkataba wake mpya. Nyota huyo na wawakilishi wake wamekataa pia kuzungumza masuala ya kuongeza mkataba mwingine baada ya huu kumalizika msimu ujao. Kuna tetesi kuwa nyota huyo amekataa kusaini mkataba mwingine kwasababu bado ana nia ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo. Rooney ameanza msimu huu akiwa katika kiwango cha juu ambapo amefunga mabao nane katika mechi 13 za Ligi Kuu alizocheza katika kikosi cha United kinachonolewa na David Moyes.

No comments:

Post a Comment