KOCHA wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann amesaini mkataba mpya wa miaka minne ambao utamfanya kuinoa timu hiyo mpaka 2018 katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi. Sehemu ya mkataba huo mpya Klinsmann pia atakuwa mkurugenzi wa ufundi wa soka wan chi hiyo. Akihojiwa Klinsmann amesema cheo cha ukurugenzi wa ufundi ni kikubwa na kina changamoto nyingi lakini atajitahidi kutumia uzoefu wake wa siku katika soka kuhakikisha anafanikisha malengo yaliyowekwa. Klinsmann aliendelea kusema kuwa atajitahidi kuhakikisha anainua timu za taifa za vijana nchini humo, kozi za makocha na kuendeleza shule za soka na anajua haitakuwa kazi rahisi. Klinsmann alianza kibarua cha kuinoa Marekani Julai mwaka 2011, akichukua nafasi ya Bob Bradley na kuingoza nchi hiyo kukata tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwakani.
No comments:
Post a Comment